Thursday, November 21, 2013

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA UCHUKUZI Dk. CHARLES TIZEBA ATEMBELEA KARAKANA YA RELI MJINI MOROGORO KUANGALIA MAENDELEO YA UUNDWAJI UPYA WA VICHWA VYA TRENI KWA AJILI YA KUIMARISHA USAFIRI WA RELI NCHINI



Muoneano wa kichwa cha treni ambacho kinaundwa Upya na Kampuni ya SMH/Rail kutoka nchini Malaysia kikiendelea kufanyiwa kazi katika karakana ya Reli mkoani Morogoro. Kichwa hicho ni moja ya vichwa ambavyo vinajengwa upya kwa ajili ya kuimarisha usafiri wa Reli Nchini. Aidha, Kichwa cha kwanza kitakabidhiwa kwa Serikali Mwanzoni mwa mwezi Disemba 2013.


Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akioyeshwa  mpango kazi wa kampuni ya SMH/Rail na Mhandisi wa Kampuni hiyo, Eng. Mohd Hisham(Kulia kwa Naibu Waziri) ambayo inaunda upya vichwa vya treni katika karakana ya Reli Mkoani Morogoro. Naibu Waziri ametembelea karakana hiyo leo Asubuhi kuangalia maendeleo ya undwaji upya wa vichwa  vya treni ambavyo viko kwenye mpango wa matokeo makubwa sasa kwenye sekta ya Uchukuzi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akiongea na vibarua walioajiriwa na kampuni ya SMH/Rail   kutoka  nchini Malaysia, asubuhi alipofanya ziara kwenye karakana ya Reli mkoani Morogoro kuangalia maendeleo ya uundwaji upya wa Vichwa vya Treni vya Shirika la Reli Tanzania(TRL). Naibu Waziri huyo amuagiza uongozi wa kampuni hiyo kuhakikisha kuwa vibarua hao wanapewa mikataba kama watafanya kazi zaidi ya miezi mitatu kama sheria za kazi zinavyowataka.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi akiongea na Naibu Mtendaji Mkuu, Uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Paschal Mafikiri (wa kwanza kushoto), wakati alipotembelea Karakana ya Reli Mkoani Morogoro, leo asubuhi kuangalia maendeleo ya undwaji upya wa vichwa vya treni. Kichwa cha kwanza kinategemea kukamilika mwanzoni mwa Mwezi wa Disemba 2013.

No comments:

Post a Comment