Wednesday, November 20, 2013

DUNIA YA SASA IMEKWISHA!




Mkuu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
  Mauaji ya aina yake yametokea Ilala Dar es Salaam leo asubuhi, kijana aliyetajwa kwa jina la Gabriel Munisi ameua watu kwa risasi na kisha akajiua. 

Vyanzo vya habari zimedai kuwa, Gabrieli alikuwa ni mfanyabiashara, na alikuwa anaishi Mwanza.Mauaji hayo yametokeo katika nyumba yenye geti jeusi jirani na baa maarufu iitwayo Club ya wazee.



Inaidaiwa kuwa, kijana muuaji alitumia teksi kwenda kwenye nyumba hiyo, akashuka akawa amesimama jirani na geti la nyumba hiyo, baada ya muda gari aina ya Toyota Surf likawa linatoka kwenye nyumba hiyo.
Muuaji huyo alitoa bastola na kuanza kulishambulia gari hilo na kumuua dereva wa gari hilo kwa kumpiga risasi kichwani, akampiga mwanamke mwingine ambaye alikuwa amepanda katika siti ya mbele, na inadaiwa kuwa amekufa.

 Inadaiwa kuwa Gabriel aliwapiga risasi abiria wawili wasichana waliokuwa wamekaa siti za nyuma ya gari hiyo,  wamejeruhiwa mabegani , baada ya hapo muuaji huyo alijipiga risasi na akafa papohapo. 

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana muda mfupi uliopita, dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo hakuuawa, aliyekufa ni kijana aliyekuwa anafungua geti ili gari hilo litoke. 

Dereva kajeruhiwa, kalazwa Muhimbili. Kwa mujibu wa Polisi, mauaji hayo ni kwa sababu ya mapenzi.Inadaiwa kuwa mlengwa mkuu kwenye shambulizi hilo ni msichana aliyetajwa kwa jina la Christina,alijeruhiwa.


Inadaiwa kuwa msichana huyo anafanya kazi benki jijini Dar es Salaam, na kwamba alikuwa ni mchumba wa Gabrieli, lakini pia alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume aliyekuwa akiendesha gari wakati tukio hilo.

Taarifa zilizopatikana zimemtaja mmoja wa waliokufa kwenye tukio hilo kuwa ni mwanamke, Alpha Alfred, alikuwa mfanyakazi wa benki ya Barclays.

No comments:

Post a Comment