Monday, November 25, 2013

NDODO ZA ULAYA






BAADA YA MAPUMZIKO YA SIKU KUMI YALIYOPISHA MICHEZO YA KIMATAIFA LIGI KUU YA ENGLAND ILIREJEA WIKIENDI HII IKISHUHUDIA LADHA YA BURUDANI YA SOKA KWA MASHABIKI WA TIMU MBALIMBALI .
EPL ILIANZIA HUKO MERSEYSIDE AMBAKO MAHASIMU WENYE URAFIKI EVERTON NA LIVERPOOL WALIKUTANA HUKO GOODISON PARK .
 HADI KIPENGA CHA MWAMUZI KUASHIRIA KUMALIZIKA KWA MCHEZO MATOKEO YALIKUWA SARE YA MABAO MATATU KWA MATATU .
LIVERPOOL WALIFUNGA MABAO YAO KUPITIA KWA FELIPE COUTINHO , LUIS SUARZ NA DANIEL STURIDGE HUKU EVERTON WAKIFUNGA KUPITIA KWA KEVIN MIRALLAS NA ROMELU LUKAKU AMBAYE ALIFUNGA MABAO MAWILI.
VINARA WA LIGI HIYO ARSENAL THE GUNNERS WALIWAFUNGA SOUTHAMPTON MABAO MAWILI BILA .
 MABAO YOTE YA THE GUNNERS YALIFUNGWA NA MSHAMBULIAJI WA KIMATAIFA TOKA UFARANSA OLIVIER GIROUD .


CHELSEA THE BLUES WAKIWA UGENINI JIJINI LONDON KWENYE UWANJA WA UPTON PARK WALIWAADHIBU JIRANI ZAO WEST HAM UNITED KWA KUWAFUNGA MABAO MATATU BILA .
SEHEMU KUBWA YA ADHABU HIYO ILITOKA KWA KIJANA WA NYUMBANI FRANK LAMPARD AMBAYE ALIFUNGA MABAO MAWILI HUKO OSCAR AKIFUNGA BAO LINGINE .

KATIKA MICHEZO ILIYOPIGWA JUMAPILI MANCHESTER CITY WAKIWA KWENYE KIWANGO CHAO BORA KWENYE UWANJA WAO WA NYUMBANI HUKO ETIHAD WALIBAMIZA TOTTENHAM HOTSPURS KWA MABAO SITA KWA SIFURI .
 MABAO YA CITY YALIFUNGWA NA JESUS NAVAS AMBAYE ALIFUNGA MABAO MAWILI , SERGIO AGUERRO NAYE AKIFUNGA MABAO MAWILI , ALVARO NEGREDO PAMOJA NA KIUNGO WA SPURS MBRAZIL ALEX SANDRO AMBAYE ALIJIFUNGA MWENYEWE.

MABINGWA WATETEZI WA LIGI HIYO MASHETANI WEKUNDU MANCHESTER UNITED WALIBANWA MBAVU MBELE YA VIJANA WALIOPANDA DARAJA WA CARDIFF CITY BAADA YA KULAZIMISHWA SARE YA MABAO MAWILI KWA MAWILI .

MABAO YA UNITED YALIFUNGWA NA WAYNE ROONEY NA PATRICE EVRA HUKU CARDIFF WAKIFUNGA KUPITIA KWA FRAZER CAMBO NA KIM BO KYUNG .
NCHINI HISPANIA TIMU ZOTE TATU KUBWA ZA LIGI HIYO ZILIPATA USHINDI MKUBWA MBELE YA WAPINZANI WAO HUKU KUKIWA NA WASTANI WA ANGALAU MABAO MANNE KWENYE KILA MECHI .
MABINGWA WATETEZI WA LIGI HIYO FC BARCELONA WALIENDELEZA MWENENDO WA MZURI WAKIWAFUNGA GRANADA KWA MABAO MANNE BILA MAJIBU .
WAFUNGAJI KWENYE MCHEZO HUO WALIKUWA CESC FABREGAS , ANDRES INIESTA , ALEXIS SANCHEZ NA PEDRO RODRIGUEZ .

MAHASIMU WA BARCA REAL MADRID WALIWAFUNGA ALMERIA MABAO MATANO BILA  .
MABAO YA WASHINDI YALIFUNGWA NA CRISTIANO RONALDO , KARIM BENZEMA , GARETH BALE , ALVARO MORATA NA ISCO .

NAO ATLETICO MADRID WALIMALIZA KARAMU YA MABAO KWA TIMU KUBWA HUKO HISPANIA KWA KUWAANGAMIZA GETAFE KWA MABAO SABA KWA SIFURI.
DAVID VILLA NA RAUL GATHIA WALIFUNGA MABAO MAWILI KILA MMOJA , ADRIAN LOPEZ NA DIEGO COSTA NA WAKAFUNGA BAO MOJA MOJA KABLA YA ADRIAN LOPO AMBAYE NI BEKI WA GETAFE HAJAJIFUNGA NA KUKAMILISHA IDADI YA MABAO SABA .
NCHINI UJERUMANI MATUMAINI YA BORRUSIA DORTMUND KUREJESHA UBINGWA WAO WA BUNDESLIGA SIKU YA JUMAMOSI YALIZIDI KUDIDIMIA  BAADA YA MABINGWA WATETEZI BAYERN MUNICH KUWAFUNGA KWA MABAO MATATU BILA .
KATIKA MCHEZO HUO WAFUNGAJI WA BAYERN WALIKUWA MARIO GOTZE AMBAYE ALIKUWA ANAKUTANA NA TIMU YAKE YA ZAMANI KWA MARA YA KWANZA , ARJEN ROBBEN NA THOMAS MUELLER .
MATOKEO HAYA YANAMAANISHA KUWA BORRUSIA DORTMUND WANASHIKA NAFASI YA TATU WAKIWA NYUMA YA VINARA BAYERN MUNICH KWA TOFAUTI YA POINTI SABA HUKU LIGI YA UJERUMANI IKIWA IMESHUHUDIA MIZUNGUKO 13 YA MICHEZO YAKE .

NCHINI ITALIA JUVENTUS WALIWAKARIBIA VINARA WA LIGI HIYO AS ROMA BAADA YA KUWAFUNGA LIVORNO MABAO MAWILI BILA .
 SAFU YA USHAMBULIAJI AMBAYO MWANZONI ILIONEKANA KUSHINDWA KUELEWANA ILIENDELEZA MFULULIZO MZURI WA UFUNGAJI KATIKA MCHEZO HUU BAADA YA CARLOS TEVEZ NA FERNANDO LLORENTE KUFUNGA MABAO YA JUVENTUS .
NCHINI UFARANSA MABINGWA WATETEZI PARIS ST GERMAIN WALICHEZA MCHEZO WAO WA 32 BILA KUPOTEZA NA SAFARI WALIVUNA POINTI ZOTE TATU BAADA YA KUWAFUNGA STADE DE REIM MABAO MATATU BILA . 
MABAO YA PSG YALIFUNGWA NA JEREMY MENEZ , LUCAS MOURA PAMOJA NA ZLATAN IBRAHIMOVIC .
AS MONACO AMBAO WALICHEZA MECHI MBILI BILA KUPATA USHINDI WALIJITUTUMUA NA KUONDOKA NA USHINDI MWEMBAMBA BAADA YA KUWAFUNGA NANTES BAO MOJA BILA .
BAO HILO PEKEE LILIFUNGWA NA MOUNIR OBADI .

No comments:

Post a Comment