Dar
es Salaam. Majiji yote matano nchini pamoja na Zanzibar na mikoa mingine kadhaa
yatakuwa na giza kwa siku kumi kuanzia leo, hivyo kusababisha adha kwa wakazi
wake.
Meneja
Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Badra Masoud, amethibitisha
kuwepo kwa adha hiyo, akielezea kuwa hali hiyo inatokana na kuzimwa kwa mitambo
ya Kampuni ya Pan African iliyopo Songosongo.
“Mitambo
hiyo itazimwa kwa sababu ya matengenezo ya lazima, hakuna jinsi ya kuzuia hali
hiyo Tanesco tunasikitika sana kwa kuwa kutakuwa na upungufu mkubwa wa umeme
kwenye gridi ya taifa,” alisema Masoud.
Alifafanua
mitambo hiyo inaendeshwa na gesi ambayo imepungua katika kisiwa hicho cha
Songosongo Wilaya ya Kilwa, Lindi.
“Upungufu
huo umesababishwa na matengenezo ya kiufundi yanayofanywa kwenye visima vya
gesi, lengo ni kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwenye visima hivyo,”
alisema.
Chanzo: mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment