Askari wa kutuliza
ghasia, FFU, wakipiga mabomu ya machozi hewani kuwatawanya mashabiki wa Simba,
waliokuwa wakifanya fujo kwa kung'oa viti na kurusha uwanjani baada ya timu ya
Kagera Sugar, kusawazisha bao lao kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 90+, iliyotolewa
na mwamuzi, Mohamed Theophile. Penati hiyo imepatikana baada ya beki wa Simba
Joseph Owini, kumchezea vibaya Daud Jumanne, penati hiyo iliyopigwa na Salum
Kanon, imezifanya timu hizo kutoka sare ya 1-1, wakati bao la SImba likifungwa
na Amis Tambwe katika dakika ya 45.
Askari wakimdhibiti
mmoja wa mashabiki wa Simba.
BAO la beki wa kulia wa
Kagera Sugar, Salum Kanoni lilipoteza amani ndani ya Uwanja wa Taifa baada ya
mashabiki wa Simba kuanza kung’oa viti hali iliyosababiosha Polisi walipue
mabomu ya machozi kutuliza vurugu hizo.
Kagera ambao walikuwa
nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Asimi Tambwe katika kipindi cha kwanza,
walipata bao la kusaweazisha kupitia kwa Kanoni kwa njia ya panalti baada ya
Joseph Owino kumwangusha Daudi Jumanne katika eneo la hatari.
Kwa sare hiyo hali ya
Simba imeendelea kuwa tyete kwani bado wamebaki katika nafasi ya nne wakiwa na
pointi 21 nyuma ya Yanga yenye pointi 22 huku Azam na Mbeya City wakiwa juu kwa
pointi 23 kila moja wakitofautiana mabao ya kufunga.
Katika mchezo huo ambao
ulikuwa na ushindani mkubwa katika dakika zote kwani timu hizo zilikuwa
zikihitaji pointi tatu ili wajiweke sehemu nzuri kabla ya kumaliza mzunguko wa
kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Simba itamalizia
mzunguko wa kwanza kwa kucheza na Ashanti United mchezo utakaochezwa kwenye
Uwanja wa Taifa, Jumamosi ya Novemba 2.
Kipa wa akiba wa Simba,
Abel Dhaila, akimlalamikia mwamuzi wa akiba baada ya mwamuzi wa kati kutoa
penati katika dakika za majeruhi.
Kipa wa akiba wa Simba, Abel Dhaila, na Kocha
Mkuu, Abdallah Kibaden, wakimlalamikia mwamuzi wa akiba baada ya mwamuzi wa
kati kutoa penati katika dakika za majeruhi.
Askari wakiendelea
kudhibiti vurugu..
Sehemu ya viti
vilivyoharibiwa....
Wachezaji wa Simba,
wakimpongeza beki wao Salum Kanon, baada ya kusawazisha bao hilo kwa mkwaju wa
penati.
Patashika langoni mwa
Kagera Sugar.
Kiungo wa Kagera Sugar,
George Kavila (kulia) akimtoka mshambuliaji wa SImba, Amis Tambwe, wakati wa
mchezo huo.
Amis Tambwe,
akidhibitiwa.
Ramadhan Singano wa
Simba (kushoto) akijaribu kumtoka beki wa Kagera Sugar, Malegesi Mwangwa.
Hatari langoni mwa
kagera.
No comments:
Post a Comment