Bwana shiyo Pamoja na Gavana wa Machakos wakiwasalimia
wachezaji.
TIMU ya Taifa ya
Tanzania Bara,Kilimanjaro Stars imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 katika
mashindno ya Cecafa Challenge yanayoendelea jijini Nairobi nchini Kenya, bao la
Said Morad aliyofuga kwa kichwa,kufuatia mpira wa kona uliopigwa na mchezaji
bora wa mechi hiyo Salum Abbakar Sure Boy, ndiyo iliyobadili ubao wa matangazo
baada ya Zambia (Chipolopolo) kuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa
Roladi Katanga.
Mfungaji alifunga bao
hilo kwa kichwa baada mabeki wa Kili Stars kushindwa kumkaba, wakati Felix
Katongo akijiandaa kupiga mpira kwenda golini, kwa matokeo hayo Kili Stars
imepata pointi moja nyuma ya Burundi inayo ongoza kundi hilo baada ya kuichapa
Somalia kwa mabao 2-0.
Wawakilishi wengine wa
Tanzania katika mashindano hayo ni Zanzibar Heroes iliyoanza vyema baada ya
kufanikiwa kuichapa Sudan Kusini kwa mabao 2-1 na kujikusanyia pointi tatu
mbele ya wenyeji Kenya na Ethiopia.
Hapa vijana wetu wakiwa katika Picha ya Pamoja Kabla ya
kwanza kwa kipindi cha kwanza.
Mtanange ukiendelea uwanja wa Machakos
Kilimanjaro Stars wakiomba dua kabla ya mchezo
Kocha wa Zambia akihojiwa na wanahabari
Mashabiki wa Kilimanjaro Stars wakishangilia timu yao
Wachezaji wa Timu yetu ya Taifa wakitoka nje ya uwanja baada ya mchezo huo
Makocha wa timu zote mbili wakihojiwa baada ya mchezo
Bwana Innocent Shiyo wa tatu kutoka kushoto wakati wa wimbo Wa Taifa wa
Tanzania ukipigwa. kulia kwa Bwana Shiyo ni Balozi wa Zambia nchini kenya Mh Josephine Mumbi
Phiri. Picha kwa Hisani ya Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya
Via: Shaffihdauda
No comments:
Post a Comment