Friday, November 8, 2013

KUTOKA MAHAKAMANI


BEFORE AND AFTER



Mwanamke huyo hapo juu aliwahi kuolewa na bwana Jian Feng ,ambaye alipatwa na udadisi baada ya kuona sura ya mtoto wake wa kwanza kwa mara ya kwanza kua ni ya kuogofya ,na kugundua kwamba ulimbwende wa mkewe ni wa kisu! (plastic surgery)

Bwana  Jian Feng alipomtazama mtoto wake mchanga kwa mara ya kwanza alipata kihoro kwani kitoto hicho cha kike kilikua kina tisha,na akashindwa kuamini kwamba yeye na mkewe mrembo wanaweza kuzaa mtoto mbaya kiasi hicho.Na ndipo hisi mbaya zikamuijia kichwani kua huenda mkewe alichepuka nje ya ndoa na kumletea kituko hicho!.
Mke alipoona mambo yamekua mambo akaamua kutapika ukweli ambao pia ulimshtua kwamba! Urembo wake ulimgharimu kiasi cha £62,000 na kama hiyo haitoshi! Hapaswi kua na mashaka na mtoto huyo kwani ni wao.

Bwana Feng alipandwa na ghadhabu na kuamua kumpandisha  courtini kwa madai ya kughilibu wakaingia ndoani na akashinda juu ya kesi hiyo .

Kauli ya Feng ni hii: “nilimuoa mke wangu bila kupenda,lakini tulipopata mtoto wetu wa kwanza,utta katika ndoa yetu ndipo ulipoanza,kwani mtoto ni mbaya sana kiasi cha kuntisha mimi babake!na akawaambia wanasheria wake kua mkewe alimlaghai kwa upasuaji alojifanyia ili aonekane mrembo lakini kuzaliwa kwa mtoto wao ndo kuliko fanya agundue siri hiyo!.
 Cha kushangaza! Mahakama ilimkubalia ombi lake na kumpa ushindi bwana Feng wa £75,000 na hii ni baada ya mkewe kukubali kuuficha ukweli wa surgery hiyo.

Kesi hiyo ilikua imeendeshwa na Jaji kutoka kaskazini mwa China . WABONGO MUPOOOOO?!!!!!!

No comments:

Post a Comment