USIKU WA ULAYA UMEWADIA KWA MARA NYINGINE AMBAPO MASHABIKI WA
SOKA DUNIANI WATAPATA FURSA YA KUTAZAMA LADHA HALISI YA MICHUANO MIKUBWA KULIKO
YOTE KWA NGAZI YA VILABU .
MICHEZO KADHAA ITAPIGWA KWENYE VIWANJA TOFAUTI AMBAPO TIMU TOKA
MAKUNDI A MPAKA D ZITAKUWA ZIKITOANA JASHO KUWANIA NAFASI YA KUFUZU KWENYE
HATUA YA 16 BORA .
KUTOKANA NA MATOKEO YA MICHEZO ILIYOPITA TIMU KADHAA ZINA NAFASI
YA KUKATA TIKETI YA KUELEKEA HATUA YA PILI ENDAPO ZITAPATA MATOKEO MAZURI HII
LEO .
TUKIANZA KWA KUTAZAMA KUNDI B , MABINGWA WA KIHISTORIA WA
MICHUANO REAL MADRID WATAJIHAKIKISHIA NAFASI YA 16 BORA ENDAPO WATAIFUNGA
JUVENTUS KWA IDADI YOYOTE ILE YA MABAO .
SI USHINDI TU
UTAKAOWAVUSHA MADRID BALI HATA SARE INATOSHA KUWAPELEKA HATUA INAYOFUATA ILI
MRADI SARE HIYO IAMBATANE NA FC COPENHAGEN KUSHINDWA KUPATA USHINDI KWENYE
MCHEZO DHIDI YA GALATASARAY.
MABINGWA WA UFARANSA PARIS ST GERMAIN WANA JUKUMU JEPESI
MIKONONI MWAO WAKATI WATAKAPOKUWA WAKICHEZA NA RSC ANDERLETCH . PSG WANAHITAJI
USHINDI WOWOTE ULE ILI KWENDA 16 BORA HUKU ZIKIWA ZIMESALIA RAUNDI MBILI ZA
MECHI.
KUNDI D LINAWEZA KUMALIZA SHUGHULI YAKE USIKU WA LEO PIA ENDAPO
VINARA WA KUNDI HILO MABINGWA WATETEZI BAYERN MUNCHEN PAMOJA NA MANCHESTER CITY
WATAPATA USHINDI KWANI VIKTORIA PLZEN NA CSKA MOSCOW WAMEJICHIMBIA KWENYE
UVUNGU WA KUNDI HILO NA HAWANA MATUMAINI YA KUFUZU HATUA INAYOFUATA .
WAWAKILISHI TOKA HISPANIA ATLETICO MADRID WATAJIHAKIKISHIA
NAFASI KWENYE 16 BORA ENDAPO WATAWAFUNGA
AUSTRIA VIENNA .
VIJANA HAO TOKA VICENTE CALDERON KATIKATI MWA JIJI LA MADRID
WANAWEZA KUFUZU PIA BILA HATA YA KUPATA
USHINDI KWANI WANAWEZA KUSONGA MBELE KWA MATOKEO YA SARE YATAKAYOAMBATANA NA FC
PORTO KUSHINDWA KUPATA POINTI TATU DHIDI YA ZENITH ST PETERSBURG .
TIMU YA MWISHO KWENYE ORODHA HII NI FC BARCELONA AMBAO WATAFUZU
ENDAPO WATASHINDA MCHEZO DHIDI YA AC MILAN .
KWA UJUMLA RATIBA YA MICHUANO HII AMBAYO KWA USIKU HUU INAINGIA
KWENYE DURU YAKE YA NNE YA MICHEZO YA HATUA YA MAKUNDI INAONYESHA KUWA KUNDI A
LITASHUHUDIA MICHEZO KATI YA REAL SOCIEDAD NA MANCHESTER UNITED PAMOJA NA
SHAKHTAR DONETSK DHIDI YA BAYER LEVERKUSEN.
KWENYE KUNDI B FC
COPENHAGEN WATAKUWA WENYEJI WA GALATASARAY HUKU JUVENTUS WAKIWA NYUMBANI
KUCHEZA NA REAL MADRID .
KUNDI C OLIMPIAKOS WATACHEZA NA BENFICA HUKU PSG WAKIWA NYUMBANI
KUCHEZA NA ANDERLETCH .
MANCHESTER CITY WATAKUWA ETIHAD KUONYESHA KAZI NA CSKA MOSCOW
HUKU VIKTORIA PLZEN WAKIWAKARIBISHA BAYERN MUNICH .
No comments:
Post a Comment