M23:
Uasi sasa basi!Kiguu na njia waasi wa M23 wamechukua silaha zao na kuondoka
ngome zao za mwisho baada ya kushindwa na jeshi la DRC.
Muasi
akiwa kashikilia mtutu
Mazungumzo
ya amani kati ya viongozi wa M23 na Serikali ya DRC yalifanyika mjini Kampala
Uganda.
Dalili
za kukaribia kushindwa kwa waasi wa M23 nchini DRC, ni ishara ya mabadiliko ya
kisiasa na mpangilio wa kijeshi ambayo yanaweka wazi matumaini ya amani katika
nchi hiyo kubwa na ambayo imekuwa na migogoro kwa miaka mingi.
Waasi
wa M23 Mashariki mwa nchi, wamepata pigo kubwa katika wiki chache zilizopita ,
na kulazimisha kiongozi wao Bertrand Bisimwa kutoa amri ya kusitisha vita na
kutaka mazungumzo ya amani kuanza tena nchini Uganda.
Ikiwa
kundi hilo litashindwa, bila shaka utakuwa ujumbe mkali kwa angalau makundi
mengine 10 ya waasi yanayoendesha harakati zao katika nchi hiyo, na kuinua
matumaini ya amani hatimaye kupatikana katika taifa hilo lenye utajiri wa
madini.
Hasa
baada ya vita hivyo kuendelea kwa miongo miwili."Kundi la M23 limekuwa
kundi ambalo harakati zake zimekuwa wazi sana Mashariki mwa nchi. Kushindwa
kwake haimaanishi ndio mwisho wa vita na mwanzo wa amani. Ni mapema mno
kutabiri hilo,’’ alisema Stephanie Wolters kutoka katika taasisi ya mafunzo ya
usalama nchini Afrika Kusini.
Ili
Kuelewa matumaini ya hatimaye kumalizika kwa vita yanatokana na nini, ni muhimu
kuelewa ambavyo waasi wa M23 wamekuwa wakiendesha harakati zao na ambavyo
walifurushwa kutoka katika ngome zao.
Wakati
waasi wa M23 walidhibiti mji wa Goma - Novemba 2012, lilikuwa jambo la aibu
sana kwa serikali ya Rais Joseph Kabila pamoja na kushinikiza jamii ya
kimataifa kuchukua hatua baada ya madai ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu
kuibuka.
Rais
Kabila alifanyia jeshi mabadiliko na dalili ya kuonyesha mambo yalikuwa
yanakwenda vyema, sababu hakuna madai zaidi ya ukiukwaji wa haki za bindamau
yaliwahi kusikika.
Machi
mwaka huu, Umoja wa Mataifa iliidhinisha kikosi cha wanajeshi 3,000 wa Afrika
waliokuwa na jukumu la kupambana na waasi.
Wanajeshi
hawa wamekuwa wakitumia ndege za helikopta kushambulia maeneo ya waasi
wakisadiana na wanajeshi wa UN (Monusco)ambao tayari walikuwa wanakabiliana na
waasi hao .
Congo
na Rwanda: Majirani mahasimuKwa sasa kuna taarifa kuwa wanajeshi wa UN
watapokea ndege zisizo na rubani, ili kufanyia uchunguzi waasi hao na ambavyo
wanaendesha harakati zao.
Umoja
wa mataifa umetuhumu Rwanda na Uganda kwa kuunga mkono waasi wa M23. Hata
hivyo, nchi hizo zimekanusha madai hayo.
Katika
kile inachosema ni nia njema ya kutaka kusaidia katika kusitisha vita DRC,
serikali ya Rais Museveni imekubali kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani kati
ya DRC na waasi wa M23
Marekani
imesitisha msaada kwa Rwanda, baada ya kuituhumu kusaidia waasi wa M23 kupiga
serikali ya DRC na ambao wanaaminika kutumia watoto kama wapiganaji wa kundi
hilo.Ni mapema sana kusema kuwa kundi la waasi wa M23 limeshindwa.
Kwa
miaka mingi serikali ya DRC imeshindwa kupambana vilivyo na makundi ya waasi
Mashariki mwa nchi, sababu moja ya hilo ni washirika wa kimataifa kujihusisha
na vita hivyo.
Serikali
ya Rais Kagame imesisitiza kuwa ilituma wanajeshi wake kusaidia serikali ya DRC
kupambana na waasi wa FDLR, kundi la waasi wa kihutu waliohusishwa na mauaji ya
kimbare ya Rwanda na ambalo linapinga ushawishi wa watutsi katika eneo hilo.
Jambo
ambalo wadadisi wanasema ni kwamba lazima serikali ya DRC iwe na mpango maalum
wa kusuluhisha tatizo la uasi katika eneo hilo la sivyo makundi ya waasi kama
FDLR ambayo yako kimya huenda yakarejea tena kuisumbua nchi hiyo baada ya M23
kuzimwa.
No comments:
Post a Comment