Mimi nikiwa Mwana
CCM na Kiongozi pia wa CCM ngazi ya Taifa na Blogger, naomba kusimama mbele ya
Mheshimiwa Mbunge Kapuya na Taifa zima la Tanzania pamoja na wasomaji wangu
wote wa Blog na meble ya Mungu, kukubali makosa na kuomba radhi, kwake na kwa
Mungu wangu zaidi. Mimi ni mmoja wa watu wa kwanza kuamini hadithi
iliyojitokeza hivi karibuni kwamba Mheshimiwa Kapuya amembaka na kumuambukiza
Ukimwi na kutishia kumuua msichana wa miaka 14.
- Leo ninaomba kusimama hapa na kusema kwamba hii habari
ni uongo na ni uzushi wa hali ya juu sana uliotengeenzwa na msichana mzoefu wa
uzushi ambaye kwanza si kweli kwamba ni Mwanafunzi, pili ni Mtumzima mwenye
mtoto tayari hata kabla hajakutana na Mh. Kapuya, pia ni muongo na mzushi
mzoefu aliyewahi kuwadanganya pamoja na Mkurugenzi wa CRDB Bank, pamoja na
kuidanganya TAMWA ambayo iliishia kumuripoti polisi na kuishia kwake kukaa
rumande Segerea kwa muda mrefu sana.
- Kwa nini niliaiamini hii hadithi ni kwamba kuna siku
mimi binafsi tulikuwa tumekaa faragha na Viongozi wengine Watatu wakubwa wa
Taifa ambapo mbunge mmoja aliyedai kuijua kwa undani hii hadithi na kuhusiaka
nayo, alianza kutuelezea hii hadithi kwa kutmia details kubwa kubwa sana,
binafsi nilikuwa ninamuamini sana yule mbunge mpaka leo nilipothibitisha kwa
100% kwamba hii hadithi haiko sawa either na yeye ni muongo wa makusudi mwenye
nia mbaya na Mh. Kapuya au na yeye alidanganywa na huyu msichana, ambaye jina
lake kamili ni Hamida as opposed na majina mengi ya uongo ambayo amekuwa
akiyatumia kudanganyia watu.
- Ninaomba kuwa wa kwanza kubeba huu msalaba, najua
kwamba sio rahisi kueleweka na wengi ambao tulishamuhukumu Mh. Kapuya, lakini
ukweli ni kwamba ni hadithi ya kutunga iliyoutngwa na msichana mmoja aliyebobea
katika uzushi na uongo wa hali ya juu sana. Majuzi Waziri mmoja ninayemuamini
sana katika Serikali ya sasa alinishitua kwamba hii hadithi ni ya uongo
niiifuatilie tena, lakini sikuamuamini mpaka leo asubuhi sana nilipopigia sim
na gazeti moja maarufu sana la Udaku, walioniambia kwamba hii habari si ya
kweli na kwamba wanaye huyu msichana pale ofisini kwao, toka asubuhi mpaka sasa
nimekuwa kwenye uhakiki wa hii ishu, na sasa ninasema wazi na tena kwamba:-
NINAMUOMBA RADHI SANA MH. KAPUYA NA NI MATUMAINI YANGU
MAKUBWA SANA KWAMBA WALE WOTE TULIOHUSIKA NA KUMHUKUMU TUTAKUBALI MAPUNGUFU
YETU KAMA WANADAMU NA KUMUUNGAMIA CHINI MUNGU WETU, NI KWELI MH. KAPUYA ALIKUWA
NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA HUYU BINTI LAKINI YA HIARI SIO KAMA ILIYOELEZWA NA
SI KWELI KWAMBA HUYU BINTI NI MWANAFUNZI, HAPANA ANA MTOTO TAYARI NA PIA
ALISHAWAHI KULIDANGANYA JESHI LA POLISI HUKO NYUMA.
- Wale wote tunahusika na media tujifunze tena na hili
fundisho, tujitahidi kuwa waadilifu na kufanya utafiti wa kina kabla ya kuruka
na hadithi nzito kama hii ambayo inaweza kummaliza mwananchi mwenzetu, au
kiongozi bila sababu za msingi wala ukweli.
- AGAIN NI MATUMAINI YANGU KWAMBA WALE TULIOHUSIKA NA
KUMHUKUMU MHESHIMIWA KAPUYA, TUTAJITOKEZA TENA IN THE PUBLIC NA KUMUOMBA RADHI
NA MSAMAHA.
- MUNGU IBARIKI TANZANIA NA KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!
WILLIAM MALECELA
No comments:
Post a Comment