Mbali ya kitunguu maji
kutumika kama kiungo katika mboga zetu, lakini pia ni tiba inayotumika sana
nchini Misri na imeonesha mafanikio kwa kutibu maradhi mbalimbali, yakiwemo
yale yasiyo na tiba katika hospitali nyingi hapa nchini.
Baadhi ya magonjwa
ambayo hadi sasa haijafahamika tiba yake katika hospitali zetu yanayotibika kwa
kitunguu maji ni pamoja na saratani (Cancer), kisukari, vidonda vya tumbo,
presha, na pumu. Dawa hii pia ni tiba ya kifua kikuu.
Kwa mujibu wa wataalamu
mbalimbali wa masuala ya tiba, kitunguu maji kina uwezo wa kufungua hamu ya
kula, hutia kiu, hulainisha chakula tumboni na huleta hamu ya tendo la ndoa kwa
wanaume na wanawake.
Aidha mtaalamu mmoja
anayefahamika kwa jina la Ibn Baitar amepata kunukuliwa akisema kwamba,
kitunguu maji huingiza kwa wingi vitamin C katika mwili wa binadamu ambayo
inasaidia sana kuona vizuri.
Lakini pia ndani ya
kitunguu maji zimo chembechembe zenye kuua vijidudu (Bacterias) na ndio maana
dawa hii ina uwezo pia wa kutibu kifua kikuu (TB), kaswendwe na kisonono.
Hivyo kupitia makala
yetu haya, tunawashauri watu wapendelee sana kutumia kitunguu maji kwa ajili ya
kinga na tiba ya maradhi katika miili yetu.
Na imethibitika kuwa
wagonjwa wengi waliowahi kutumia tiba ya kitunguu maji kwa muda mrefu wamepata
nafuu na wengine hupona kabisa maradhi yao.
Sasa ebu tuangalie
matumizi sahihi ya dawa ya kitunguu maji;
Kwa mgonjwa wa kifaduro,
pumu, vidonda vya tumbo, presha, kifua kikuu, malaria na ugonjwa wa matumbo
(typhold) anatakiwa mgonjwa kuchukua juisi ya kitunguu maji ujazo wa kikombe
cha kahawa achanganye na asali mbichi ujazo wa nusu lita, kisha aitumie kwa
kula katika ujazo wa kijiko kikubwa asubuhi na jioni.
Ama wale wagonjwa
wanaosumbuliwa na matatizo ya nguvu za kiume wanashauriwa watafune kitunguu
maji kibichi kwa muda wa siku saba asubuhi na jioni.
Na maradhi yote
yaliyobakia yanatibika kwa njia mbili zifuatazo;- kwanza kwa njia ya kiungo
katika mboga na pili ni kwa kutafuna kitunguu chenyewe kila siku na Mola Muumba
akipenda matatizo yatapungua ama kwisha kabisa.
Aidha kwa mgonjwa wa
mapunye na kunyonyoka nywele kichwani anaweza kujitibu kwa kukipondaponda
vizuri, alafu achanganye na mafuta ya zaituni, kisha apake kichwani mpaka
atakapoona tatizo limekwisha.
No comments:
Post a Comment