MICHEZO YA KUSAKA TIKETI YA KUFUZU MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA ITAKAYOFANYIKA NCHINI BRAZIL MWAKANI IMEENDELEA KATIKATI NA MWISHONI MWA WIKI ILIYOPITA .
KATIKA MICHEZO HIYO AMBAYO INACHEZWA KWA MTINDO WA MTOANO URUGUAY WALIWAFUNGA JORDAN MABAO MATANO KWA SIFURI .
WAFUNGAJI WA URUGUAY WALIKUWA EDINSON CAVANNI , MAXI PEREIRA CHRSTIANI STUANI,NICOLAS LODEIRO NA CHRSTIAN RODRIGUEZ.
KATIKA MCHEZO MWINGINE MEXICO AMBAYO ILIKUWA INAWATUMIA WACHEZAJI WA NYUMBANI PEKEE ILIWAFUNGA NEW ZEALAND MABAO MATANO KWA MOJA .
MABAO YA MXICO YALIFUNGWA NA ORIBE PERALTA AKIFUNGA MABAO MAWILI , RAFAEL MARQUEZ , PAU AGUILAR NA RAUL JIMENEZ HUKU BAO PEKEE LA NEW ZEALAND LIKIFUNGWA NA CHRISTIAN JAMES .
BARANI ULAYA KULIKUWA NA MICHEZO MINNE YA HATUA YA MTOANO AMBAYO ILIKUWA INASAKA TIMU NNE ZITAKAZOUNGANA NA TIMU TISA AMBAZO TAYARI ZIMESHAFUZU.
URENO WAKIWA NYUMBANI WALIWAKARIBISHA SWEDEN KATIKA MCHEZO ULIOISHA KWA USHINDI WA BAO MOJA BILA .
BAO PEKEE LILIFUNGWA NA NAHODHA WA TIMU HIYO CRISTIANO RONALDO.
MABINGWA WA ULAYA KWA MWAKA 2004 MABAHARIA WA UGIRIKI WALIWAFUNGA ROMANIA MABAO MATATU KWA MOJA .
WAFUNGAJI WA UGIRIKI WALIKUWA KOSTAS MITROGLOU AMBAYE ALIFUNGA MABAO MAWILI NA DIMITRIS SALPINGIDIS HUKU ROMANIA WAKIFUNGA KUPITIA KWA BOGDAN STANCU.
UKRAINE WALIUSHANGAZA ULIMWENGU KWA KUWAFUNGA UFARANSA KWA MABAO MAWILI BILA .
MABAO YA WASHINDI YALIFUNGWA NA ROMAN ZOZULYA NA ANDRIY YAMOLENKO.
BARANI AFRIKA MICHEZO YA MARUDIANO YA MTOANO WA KUFUZU KOMBE LA DUNIA ILIPIGWA KWENYE SIKU ZA JUMAMOSI NA JUMAPILI . TIMU YA TAIFA YA NIGERIA IKIWA KWENYE NGOME YAKE YA KUAMINIKA HUKO CALABAR ILIWAFUNGA ETHIOPIA MABAO MAWILI BILA .
WAFUNGA WA NIGERIA WALIKUWA OBINNA NSOFOR NA VICTOR MOSES.
MATOKEO HAYO YANAMAANISHA KUWA NIGERIA WALIKUWA TIMU YA KWANZA TOKA BARANI AFRIKA KUFUZU KOMBE LA DUNIA KWA JUMLA YA MABAO MANNE KWA MAWILI.
KATIKA MCHEZO MWINGINE IVORY COAST NA SENEGAL WALITOKA SARE YA BAO MOJA KWA MOJA .
MOUSSA SOW ALIIFUNGIA SENEGAL BAO LAO KWA MKWAJU WA PENATI KABLA YA SALOMON KALOU HAJASAWAZISHA BAO HILO .
IVORY COAST WALIUNGANA NA NIGERIA WAKIWATOA SENEGAL KWA JUMLA YA MABAO MANNE KWA MAWILI.
CAMEROON WAKIWA NYUMBANI KWAO KWENYE UWANJA WA OMNISPORT WALIWAFUNGA TUNISIA MABAO MANNE KWA MOJA .
MABAO YA CAMEROON YALIFUNGWA NA JEAN MAKOUN AMBAYE ALIFUNGA MABAO MAWILI , PIERRE WEBBO NA BENJAMIN MOUKANDJO .
MATOKEO HAYO YANAWAFANYA CAMEROON KUUNGANA NA NIGERIA PAMOJA NA IVORY COAST .
ENGLAND WAKIWA KWENYE UWANJA WA WEMBLEY WALIKUBALI KIPIGO CHA MABAO MAWILI BILA MBELE YA CHILE .
MABAO YA CHILE YALIFUNGWA NA NYOTA WA BARCELONA ALEXIS SANCHEZ AMBAYE ALIFUNGA MABAO YOTE MAWILI.
KWINGINEKO ITALIA NA UJERUMANI WALIKUTANA KATIKA MCHEZO ULIOISHA KWA SARE YA BAO MOJA KWA MOJA .
MABAO YA MCHEZO HUO YALIFUNGWA NA MABEKI AMBAPO UJERUMANI WALIFUNGA KUPITIA KWA MATS HUMMELS NA ITALIA WAKASAWAZISHA KUPITIA KWA IGNAZIO ABATE .
COLOMBIA WALIWAFUNGA UBELGIJI MABAO MAWILI BILA .
RADAMEL FALCAO NA SEGUNDO IBARBO .
JAPAN NA UHOLANZI WALITOKA SARE YA MABAO MAWILI KWA MAWILI .
UHOLANZI NDIO WALIOANZA KUFUNGA KUPITIA KWA RAFAEL VAN DER VART NA ARJEN ROBBEN NA JAPAN WAKASAWAZISHA KUPITIA KWA YUYA OSAKO NA KEISUKE HONDA .
TIMU YA TAIFA YA HISPANIA ILIKUWA BARANI AFRIKA AMBAKO ILICHEZA NA EQUATORIAL GUINEA .
KATIKA MCHEZO HUO HISPANIA ILISHINDA MABAO MAWILI KWA MOJA .
SANTI CAZORLA NA FRANSCISCO JUAN FRAN NDIO WALIOFUNGA MABAO YA HISPANIA HUKU JIMMY BERMUDEZ AKIIFUNGIA GUINEA BAO PEKEE.
WENYEJI WA MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA BRAZIL WALIWAFUNGA HONDURAS MABAO MATANO BILA .
MABAO YA BRAZIL YALIFUNGWA NA DANTE , BERNAD , MAICON, WILLIAN NA HULK.
No comments:
Post a Comment