Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (wa tatu kutoka kulia), akiongea
na fundi ambaye anafanya shughuli za ujenzi katika Daraja la Reli la
Bahi-Kintinku. Dk. Charles Tizeba amefanya ziara kwenye daraja hilo na kupata taaarifa kuwa limekamilika kwa
asilimia 98. Aidha daraja hilo limegharimu
kiasi cha Shilingi Bilioni 3.5.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (wa pili kutoka mbele), akishuka
chini ya daraja la bahi-kintinku kuangalia maendeleo ya ujenzi wake. Daraja
hilo linajengwa na Kampuni ya China Civil Engineering Construction
Corporation(CCECC).
Kukamilika kwa daraja hilo kutasababisha Treni za abiria na mizigo kupita kwa
uhakika majira yote ya mwaka.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, akitoa maelekezo kwa Mhandisi
Mkazi wa mradi kutoka kampuni ya China Civil
Engineering Construction Corporation(CCECC),
Bw. Wang Chao(aliyevaa fulana ya rangi ya karoti), wakati alipotembelea mradi
huo mapema wiki hii. Ujenzi wa daraja hilo umekamilika kwa asilimia 98 na
litakabidhiwa kwa Serikali mapema tarehe 28 Novemba 2013.
Muonekano
wa daraja la reli linalojengwa na kampuni ya China Civil Engineering Construction
Corporation(CCECC) katika
eneo la Bahi mkoani Dodoma. Kukamilika kwa daraja hilo kutawezesha treni ya
reli ya kati kupita kwa majira yote ya Mwaka. Aidha daraja hilo limekamilika
kwa asilimia 98.
Mafundi
wakiendelea na ukamlilishaji wa daraja la Reli la Bahi-kintinku kama
walivyokutwa mapema wiki hii katika eneo la bahi mkoani Dodoma. Daraja hilo
ambalo lina tani 32 litawezesha treni la Abiria na mizigo kupita kwa majira
yote kwa uhakika.
No comments:
Post a Comment