Raisi Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia.
Kiongozi msafara wa
raisi wa Liberia amekamatwa akihusishwa pamoja na kutuhumiwa kuvuda mihadarati
kwenye gari mojawapo la msafara wa rais taarifa hii imetolewa na kitengo cha
kuzuia dawa za kulevya nchini Liberia Drug Enforcement Agency (DEA).
Kiongozi huyo anaitwa Perry
Dolo alikamatwa akiwa na kilo 297 za marijuana
baada ya kuvuka boda kuelekea Sierra Leone, imefahamika.
Gari iliyokua imebeba
mzigo huo ilikua ni aina ya iliyokua inatumika kama "Escort 1", ambayo mara zote huongoza
msafara wa raisi Ellen Johnson Sirleaf.
Na siku alipokamatwa Mr
Dolo alikua katika siku ya mapumziko ama day off, na alikua akilitumia gai hilo.Na
mpaka sasa Dolo hajazungumza lolote kuhusiana na shutuma hizo.
Mr Dolo alikamatwa
pamoja naye watu wengine wenye uraia wa Liberi, Guine na mtu wa tatu
inasemekana ni mmoja kati ya askari jeshi wa
nchi ya Sierra Leone.
Mkuu wa kitengo cha
kuzuia dawa za kulevya nchini Liberia bwana Anthony Souh amesema watuhumiwa
wote wako chini ya ulinzi
Tukiwahoji kuhusiana na
tuhuma hizo, na tunataka kuharakisha uchunguzi ili ikibainika kwamba wanahusika
na kashfa hiyo wafikishwe mahakamani haraka iwezekanavyo!kwakua kesi
inayowahusi ni kubwa kwa kutumia gari ya raisi? Ni kesi kubwa!
Inasemekana Mr Dolo alikua
anafuatiliwa kwa muda wa wiki 2 yeye na wenziwe hao na ndipo walipoingia kwenye
kumi na nane mwishoni mwa wiki wakiwa mapumziko katika mji wa Tienne,kama
kilomita t 20km mili 12 katika mji wa Liberia
mji ulioko kaskazini mwa mji mkuu wa, Monrovia.
Pili inasemekana siku
hiyo Mr Dolo hakua kazini siku hiyo lakini bado alikua anatumia gari hilo
alieleza Mr Souh .
Kukamatwa kwa Mr Dolo
ni mkakati wa nchi hiyo ya Liberia katika miaka ya karibuni ulioongezwa nguvu
kusaka na kuteketeza mashamba yalimayo marijuana yaliyoko mashambani ingawa
kitengo hicho kinakabiliwa na vitendea kazi kuwafikia wakulima.
Kwa muujibu wa ripoti
iliyotolewa na ofisi ya umoja wa mataifa inayojihusisha na dawa za kulevya na
makosa ya jinai imeeleza kwamba 9% ya
wanafunzi wa Liberia walioko sekondari wana tumia dawa hiyo
Pamoja na hilo Liberia
inajitahidi kuponya majeraha ya baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe ambayo
ilisitishwa muongo mmoja uliopita.!
No comments:
Post a Comment