Dk Sengodo Mvungi
Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa
NCCR-Mageuzi, Dk Sengodo Mvungi amefariki dunia leo alasiri nchini Afrika
Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa
ni majambazi.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mwenyekiti Taifa
wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Dk Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Novemba 13, mwaka huu
nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa
Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya
Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini.
Dr Sengondo Mvungi enzi za uhai wake!
Chanzo: mwananchi.co.tz
Chanzo: mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment