Thursday, November 7, 2013

UNIC NA YUNA WATEMBELEA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO MBALIMBALI JIJINI ARUSHA

IMG_2521
Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakiwa kwenye mazungumzo ya awali na Mkuu wa Shule ya Arusha (Madam Kitigwa) baada ya kuwasili katika shule hiyo kwa lengo la kukutana na Kilabu cha Umoja wa Mataifa shuleni hapo na kuzungumza na Wanafunzi kuhusiana na agenda mbalimbali za Umoja huo. Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa kikishirikiana na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA) wapo katika ziara ya kuzitembelea shule zenye na zisizo na Vilabu vya Umoja huo kwa lengo la kufikisha habari na kazi za Umoja wa Mataifa.

IMG_2563
Afisa Habari wa Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi-wananchama wa klabu ya Umoja wa Mataifa katika Shule ya Msingi Arusha Medium ambapo amewasisitiza juu ya umuhimu wa kuzifahamu agenda mbalimbali za Umoja Mataifa na nafasi yao katika kuleta maendeleo chanya kwa jamii.
IMG_2602
Mwenyekiti Taifa wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa Tanzania Bara na Visiwani (UNCTN) Bw. Rahim Rajab Nasser akizungumza na vijana wa shule ya msingi Arusha Medium juu ya umuhimu wa vilabu hivyo na umuhimu wa ushiriki wao kuanzia shule za msingi mpaka Sekondari na Vyuoni.
IMG_2629
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama (katikati) akisisitiza jambo kwa vijana wa shule ya msingi Arusha Medium. Kulia ni Mkutubi wa Maktaba ya kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Harriet Macha na kushoto Mwenyekiti Taifa wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa Tanzania Bara na Visiwani (UNCTN) Bw. Rahim Rajab Nasser.
IMG_2650
Kobe mwenye umri sawa na shule ya Msingi Arusha Medium iliyojengwa mwaka 1930 akiwa hai mpaka na kuwa kivutio kwa wageni mbalimbali wanaofika shuleni hapo ikiwemo Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN).
IMG_2754
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha kuhusiana na umuhimu wa agenda za malengo ya Milenia (MDG's) yanayotarajia kufikia tamati 2015 ambapo wao kama vijana wameshauriwa kutilia mkazo utekelezaji wa malengo hayo ikiwemo Usawa wa kijinsia na fursa sawa kwa Wanawake, Upatikanaji wa Huduma bora za uzazi na kupambana na Ukimwi, Malaria na magonjwa mengine.
IMG_2748
Pichani juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha waliobahatika kushiriki mkutano huo ulioendeshwa na Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN).
IMG_2782
IMG_2860
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama akisalimiana na Mkuu wa Shule ya USA Academy Bw. Elibariki Malisa mara baada ya kuwasili shuleni hapo. Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa kikishirikiana na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA) wapo katika ziara ya kuzitembelea shule zenye na zisizo na Vilabu vya Umoja huo kwa lengo la kufikisha habari na kazi za Umoja wa Mataifa.
IMG_2868
Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakiwa na mwenyeji wa msafara wao MC Kalinga wa Arusha wakielekea kukutana na wanafunzi wa USA Academy.
Kwa picha zaidi ingia hapa

No comments:

Post a Comment