Ni kesho, kazi ni kwako
Sauda Simba Kilumanga
UMOJA WA ULAYA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
European Film Festival
2013, bonanza la filamu mwishoni mwa wiki
Tamasha la Filamu za Ulaya mwaka 2013 litaanza rasmi
Ijumaa tarehe 22 kwa kuonyesha filamu "Untouchables", kutoka Ufaransa
katika ukumbi wa Alliance Française saa mbili kamili usiku.
"Untouchables," filamu iliyofanya vizuri kwa
mauzo, iliyotayarishwa mwaka 2011, imewekwa katika mandhari ya Paris na inahusu
mabadiliko katika maisha ya msomi kutoka familia inayoheshimika, pindi maisha
yake yanapokutana na maisha ya Muafrika, ambaye amemfata ili kumwekea sahihi
katika nyaraka yake ya uhifadhi wa jamii (social security) ili aweze kupata
mafao yake.
Filamu hii imekuwa ikielezewa kuwa ni filamu
iliyochangamka, yenye kutia moyo na yenye mguso katika masuala ya ulemavu na
rangi lakini muhimu zaidi, ni filamu kuhusu urafiki.
"Tuna furaha sana kuwaletea filamu hii nzuri katika
ufunguzi kwa kupitia Tamasha la Filamu za Ulaya ambayo, ingawa ina muonekano
mwepesi, ni filamu inayoangalia hali halisi ya ulemavu na urafiki wa watu
wasiolingana," alisema Balozi wa Umoja wa Ulaya Filiberto Ceriani
Sebregondi.
Filamu 18 zitaonyeshwa mwaka huu katika kumbi nne,
Century Cinemax - Mlimani City , Nafasi Art Space, Goethe - Institut na
Alliance Française – zote bila kiingilio.
Tamasha la Filamu za Ulaya lilianzishwa ili kukuza uelewa
wa utamaduni kati ya Ulaya na nchi washirika wake. Kuna matamasha mengi ya
filamu za Ulaya duniani kote na jijini Dar es Salaam tamasha hili limekuwa
likifanyika kila mwaka tangu mwaka 1990.
"Ulimwengu unazidi kuwa sehemu ndogo sana lakini
bado tunashikilia utambulisho wetu wa kiutamaduni. Filamu ni njia nzuri ya
kuonyesha jinsi jamii zinavyoishi kwa namna tofauti na wanavyoshirikiana lakini
pia kuonyesha jinsi gani wanafanana. Tuna furaha kuwaletea watanzania na wageni
wanaoishi Dar es Salaam filamu za kusisimua bila kiingilio mwishoni mwa wiki
hii na tunatarajia mahudhurio mazuri,'' alisema Balozi Sebregondi.
Mwaka huu, tamasha linahusisha maigizo, vichekesho,
makala na uhuishaji (animation). Filamu zitakazoonyeshwa mwishoni mwa wiki
kuanzia tarehe 22 mpaka 24 zitakuwa kwa ajili ya watu wazima na watoto kwa
pamoja.
Baadhi ya filamu zilizochaguliwa zinagusa moja kwa moja tamaduni
za Kiafrika, kama vile The Captain of Nakara, iliyodhaminiwa na Umoja wa Ulaya,
na The Marshal of Finland kutoka Finland. Nyingine zinatoa mwanga juu ya mifumo
ya maisha ya Ulaya kwa wahamiaji au familia za vizazi vya pili.
Nchi zinazoshiriki ni pamoja na Ireland, Ufaransa,
Italia, Uswisi, Slovakia, Norway, Hispania, Uholanzi, Ubelgiji , Jamhuri ya
Czech , Uingereza, Ujerumani, Denmark, Sweden na Finland. Ujumbe wa Umoja wa
Ulaya pia huchangia filamu.
Maelezo
Mratibu wa Tamasha la Filamu:
Bi Lucian Schim van der Loeff 0652803306 na Bi Kulthum
Issa 0767954679
Kwa ratiba na habari kuhusu filamu tembelea:
http://efftanzania.wordpress.com/
No comments:
Post a Comment