Mwenyekiti wa Chama cha
Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba ameongea na waandishi wa habari siku ya
Jumapili 10 Novemba 2013 katika ofisi za makao makuu ya CUF zilizopo Buguruni
jijini Dar es salaam, Profesa Lipumba amesema kwamba wanaunga mkono Tanzania
kutojitoa kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hayo yamefuatia kutokana na
vuguvugu lilikuwepo kwamba Tanzania imekuwa haishirikishwi kikamilifu katika
mikutano iliyofanyika bila Tanzania kushirikishwa na kufuatia mawaziri kutoa
matamko mbalimbali ambayo ingepelekea kujitoa katika Jumuiya hiyo.
Siku ya
Alhamisi 7 Novemba 2013 Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dokta Kikwete
aliutubia bunge na kutoa msimamo wa Tanzania katika Jumuiya hiyo kwamba
Tanzania haitajitoa katika Jumuiya hiyo.
Toa Maoni Yako
No comments:
Post a Comment