Friday, November 15, 2013

WENYE SURA MBAYA TWENDE WAPI? HII SI SAWA




Wanawake wenye mvuto na urefu wa kuridhisha na maumbo ya kuvutia ndio wenye daraja la kwanza na kujihakikishia nafasi za kazi katika shirika la ndege la China a.k.a Chinese airline.
 


Haijalishi ikiwa CV  yako haiku poa kiviiile! Ama hata kama itakua inatisha na unaakili kiasi cha kuitwa genius! Kama huna mvuto wa sura,umbo la kuita na urefu wa twiga! Imekula kwako! Maana huna sifa za kufanya kazi katika Chinese airline.

Maelfu ya walokua hawana ajira, walijaribu bahati zao siku za hivi karibuni! Katika mji wa Shanghai ili kupata nafasi ya kazi ambazo ni za ndoto zao kua ma-air hostess lakini walielezwa mapema kabisaaa kua kamawata kidhi viwango basi watalamba nafasi za kazi.

Na wale wote wenye viwango watalazimika kupimwa urefu wa sura zao ili kukamilisha viwango,vigezo na masharti kuzingatiwa,pia walitakiwa kufanya jaribio la kunyoosha mabega yao ama lah.walitazamwa pia kama wana makovu,kuungua ungua na kasoro zinginezo kabla ya kuendelea na hatua ingine ya interview

Mtazamo ama muonekano ni muhimu sana katika utamaduni wa China na si kawaida ya muajiri kuomba upeleke picha zako!vipimo ama hata cheti za ndoa pindi watangazapo nafasi za kazi.

Spring Airlines  hivi karibuni iligoma vichwa na vyombo vya habari huko China baada ya kufanya mabadiliko ya mtindo wa interviews zake za kiuajiri na kuruhusu wanawake wenye umri wa miaka kujiunga na shirika hilo kufanya kazi,na wao wameona kua mabadiliko hayo si lolote wala si chochote kawaida tu!.
 

No comments:

Post a Comment