Friday, November 29, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA SHEREHE ZA MAADHIMISHO MIAKA 10 YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA), DAR ES SALAAM.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hituba yake ya uzinduzi rasmi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Miaka 10 ya Mapinduzi katika Sekta ya Mawasiliano Tanzania, yaliyozinduliwa rasmi  katika Ukumbi wa Mliman City,jijini Dar es Salaam.
 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Prof. John Nkoma, wakati alipotembelea katika chumba cha Mtambo wa Kufuatilia Mawasiliano ya Simu (Telecommunicatins Traffic Monitoring System) baada ya kufungua rasmi Sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi msaidizi Chumba cha Mtambo wa Kufuatilia Mawasiliano ya Simu (Telecommunicatins Traffic Monitoring System) Sunday Richard, wakati alipotembelea chumba hicho baada ya kufungua rasmi Sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa (wa pili kulia) ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Prof. John Nkoma.
 Maelezo zaidi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akizungumza na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Prof. John Nkoma (kulia) na Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa, nje ya Jengo la Mawasiliano baada ya kutembelea Chumba cha Mtambo wa Kufuatilia Mawasiliano ya Simu (Telecommunicatins Traffic Monitoring System) baada ya kufungua rasmi Sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam..
 Baadhi ya wafanyakazi wa TCRA
Wana TCRA


Makamu wa raisi na baadhi ya wafanyakazi wa TCRA katika picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment