Mwenyekiti wa Darts Mkoa wa Mbeya, Weston Asisya aliyesimama alisema baada ya kupokea mwaliko wa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo kwa mwaka huu kutoka Darts taifa tayari maandalizi ya viwanja yameshakamilika
katibu wa Chama hicho
Mkoa wa Mbeya, Anna Mwakabonga wapili kushoto
alisema mbali na maandalizi ya kitaifa pia timu ya Mkoa imeandaliwa
vizuri kuhakikisha inafanya vizuri ikiwa nyumbani.
Baadhi wa wachezaji
wanaounda timu ya Darts Mkoa wa Mbeya, Raymond Mushi alisema mazoezi
wanayoendelea kuyafanya pamoja na kikosi kilichoundwa wapinzani wajue watakuja
Mbeya kutalii tu.
MASHINDANO ya mchezo wa
vishale (Darts) kitaifa yanatarajia kufanyika Mkoani Mbeya kuanzia Novemba 23
hadi Novemba 24, mwaka huu.
Akizungumzia hali ya
maandalizi ya michuano hiyo, Mwenyekiti wa Darts Mkoa wa Mbeya, Weston Asisya
alisema baada ya kupokea mwaliko wa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo kwa mwaka
huu kutoka Darts taifa tayari maandalizi ya viwanja yameshakamilika.
Alisema michuano hiyo
itafanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Kiwira iliyopo Jijini Mbeya ambapo jumla
ya Mbao za kuchezea 12 zimeshafungwa tayari kwa mashindano.
Alisema Mbeya itakuwa
mara ya pili kuandaa mashindano kama hayo kitaifa ambapo mara ya kwanza
yalifanyika mwaka 2010 na yalikuwa na mafanikio makubwa hali iliyowavutia
kuandaa tena.
Alisema katika
mashindano ya mwaka huu yanatarajia kushirikisha mikoa 12 yenye timu za vishale
ikiwa na wachezaji zaidi ya 150 Wanawake kwa wanaume ambapo Mkoa wa Mbeya
unatakiwa kuandaa timu nne kama mwenyeji.
Alisema kutokana na
ukubwa wa Mkoa wa Mbeya wameteua Wilaya ya Rungwe kuwakilishwa kama mkoa ambao
utaopaswa kuandaa timu mbili huku Mbeya Mjini nao ukibakia na timu mbili.
Kwa upande wake katibu
wa Chama hicho Mkoa wa Mbeya, Anna Mwakabonga alisema mbali na maandalizi ya
kitaifa pia timu ya Mkoa imeandaliwa vizuri kuhakikisha inafanya vizuri ikiwa
nyumbani.
Alisema wamejipanga
vizuri kuhakikisha timu ya mkoa inaibuka na ushindi mnono tofauti na mashindano
ya mwaka jana yaliyofanyika kitaifa Mkoani Mwanza ambapo timu ya Wanawake ya
Mkoa wa Mbeya iliibuka kidedea kwa kujinyakulia kombe la mshindi wa pili.
Baadhi wa wachezaji
wanaounda timu ya Darts Mkoa wa Mbeya, Raymond Mushi alisema mazoezi
wanayoendelea kuyafanya pamoja na kikosi kilichoundwa wapinzani wajue watakuja
Mbeya kutalii tu.
Alisema wamejipanga
kuhakikisha wanachukua ubingwa katika kila raundi watakayocheza na kwamba
wachezaji wengi ni wazoezi na wamecheza vishale kwa muda mrefu hivyo hawaoni
sababu ya kushindwa.
No comments:
Post a Comment